Ligi ya Championship Tanzania Bara msimu wa 2025/26 inaanza leo, ambapo Kagera Sugar watamenyana na Transit Camp kwenye Uwanja wa Kaitaba, wakati Mbuni FC wakiwaalika Mbeya Kwanza jijini Arusha.
Kocha wa Kagera, Juma Kaseja, amesema lengo ni kushinda mechi mbili za kwanza nyumbani ili kurudisha timu Ligi Kuu.
“Tulishuka wote, tunapanda wote. Pointi sita nyumbani ni lazima,” alisema.
Kocha wa Transit Camp, Shadrack Nsajigwa, amesema wanajua ugumu wa mchezo lakini hawatoki bila pointi.