Friday, December 12, 2025
spot_img
HomeElimuKibaha Manispaa yakabidhi baiskeli kumsaidia mwanafunzi mwenye ulemavu kufika shuleni

Kibaha Manispaa yakabidhi baiskeli kumsaidia mwanafunzi mwenye ulemavu kufika shuleni

Manispaa ya Kibaha imemkabidhi baiskeli kijana mwenye ulemavu, Goodluck Mchome, mkazi wa Kata ya Kibaha Mwendapole na mwanafunzi wa Darasa la Pili katika Shule ya Msingi Tumbi, ili kumsaidia kufika shuleni kwa urahisi pamoja na kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, ambapo Mkurugenzi Dk. Rogers Shemwelekwa alimkabidhi rasmi baiskeli hiyo kwa niaba ya Manispaa.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Dk. Shemwelekwa alisema Serikali itaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali ya mwanafunzi huyo na kuhakikisha baiskeli hiyo inakuwa katika hali nzuri muda wote ili kumwezesha kufika shuleni bila matatizo.

“Tutaendelea kuhakikisha baiskeli hii inakuwa katika hali nzuri. Ikiharibika muda wowote, tutaitengeneza ili Goodlack aendelee kupata elimu bila kikwazo chochote,” alisema Dk. Shemwelekwa.

Kwa upande wake, mama mzazi wa Goodlack, Jaqueline Mbwambo, aliishukuru Manispaa ya Kibaha kwa msaada huo, akisema umeondoa changamoto ya usafiri iliyokuwa ikimkabili mwanawe kwa muda mrefu.

“Namshukuru sana Rais Samia na Manispaa ya Kibaha kwa kutatua changamoto ya usafiri iliyokuwa ikimzuia mwanangu kwenda shule kwa wakati. Sasa ataweza kusoma kwa amani na kufikia ndoto zake,” alisema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments