Sunday, March 29, 2026
spot_img
HomeMichezoMotsepe atangaza ziara Senegal, Morocco ishi ya Kombe AFCON

Motsepe atangaza ziara Senegal, Morocco ishi ya Kombe AFCON

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ametangaza kuwa anatarajia kufanya ziara rasmi katika nchi za Senegal na Morocco kwa lengo la kukutana na viongozi wa serikali pamoja na wadau wa soka katika mataifa hayo.


Akizungumza kuhusu umuhimu wa mshikamano kupitia mchezo wa soka, Motsepe alisisitiza kuwa CAF haitaruhusu mchezo huo kutumika kama chanzo cha migawanyiko miongoni mwa wananchi. Alieleza kuwa dhamira ya shirikisho hilo ni kuhakikisha soka linakuwa chombo cha kuunganisha watu na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa hayo mawili.


‎“Hatutaruhusu mpira wa miguu kuwagawanya watu wetu na kuleta dhiki na mvutano. Soka lazima liwe daraja la kuwaunganisha wananchi wetu. CAF na mimi binafsi tumejizatiti kuhakikisha uhusiano mzuri kati ya watu wa Senegal na Morocco unaendelea kudumishwa na kuimarishwa,” alisema Motsepe.


‎Katika hatua nyingine, Motsepe alitangaza maboresho makubwa katika michuano ya Africa Cup of Nations (AFCON), akibainisha kuwa kuanzia mwaka 2028, idadi ya timu zitakazoshiriki itaongezeka kutoka 24 hadi kufikia 28. Hatua hiyo inalenga kuongeza ushindani, kutoa fursa zaidi kwa mataifa mengi kushiriki, pamoja na kukuza kiwango cha soka barani Afrika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments