Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limesema matokeo ya uchunguzi walioufanya na kwa kupitia vielelezo walivyofanikiwa kuvipata umethibitisha kuwa Padri Camillus Nikata hakuwa ametekwa bali alikuwa ‘amejiteka’ na amepatikana akiwa hai katika mashamba ya Mtyangimbole yaliyopo halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani humo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Marco Chilya chanzo cha ‘kujiteka’ huko ni msongo wa mawazo.




