Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea kuongeza muda wa uchukuaji wa fomu katika kile kilichoelezwa kutoa muda zaidi kwa wanachama upande wa Bara kuchukua fomu za kugombea udiwani, ubunge na Urais.

Katika barua yake ya tarehe 1 Agosti 2025 kwenda kwa Makatibu wa Mikoa Majimbo na Kata, Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu ameeleza uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Uongozi ya Taifa kuwapa fursa wanachama.