Sunday, March 22, 2026
spot_img
HomeHabariAskofu Libena: Watanzania tulinde amani ya Taifa Letu

Askofu Libena: Watanzania tulinde amani ya Taifa Letu

Askofu wa Jimbo Katoliki Ifakara, Mhashamu Sulutaris Libena amewataka Watanzania kulinda na kudumisha amani na kuzingatia makubaliano na maelewano, kwa kuwa ndiyo msingi wa amani wa Taifa lao.

“Sisi kama nchi tunafurahia amani, tunasema tuna amani na ni kweli tuna amani. Hatuna vita hatuna magomvi, amani iendane na upendo, iwe zao la ukweli na amani inatokana na upendo.  Amani inahitaji sana makubaliano na maelewano,” amesema Askofu Libena.

Askofu Libena ameyasema hayo Aprili 20, 2025, alipokuwa akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Pasaka kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Mtume, Jimbo Katoliki lililopo Ifakara, mkoani Morogoro.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments