Azam yalenga CAF, yajiandaa na KenGold

Kocha Mkuu wa Azam FC, Rashid Toussi, ameweka wazi kuwa wataingia kwa tahadhari katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KenGold utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya.

Licha ya KenGold kushika mkia kwenye msimamo wa ligi, Toussi amesema wanawaheshimu wapinzani wao na wanatambua mchezo hautakuwa rahisi. Amesisitiza kuwa maandalizi mazuri, ikiwemo mechi za kirafiki kipindi cha mapumziko ya FIFA, yamewasaidia kuimarisha kikosi chao.

Kwa upande wake, Kocha wa KenGold, Omary Kapilima, amesema wamejipanga kupata ushindi licha ya matokeo mabaya ya nyuma, na wana matumaini ya kubadilisha hali yao kwenye msimamo wa ligi.

Mechi nyingine za ligi hiyo leo zinahusisha JKT Tanzania dhidi ya Dodoma Jiji, huku Kagera Sugar wakiwakaribisha Coastal Union Kaitaba. Jana, Pamba Jiji ililazimishwa sare ya 1-1 na Namungo FC, matokeo yaliyoifanya Namungo kufikisha pointi 24, huku Pamba Jiji ikiwa na 23.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *