Aziz Ki, Sillah wakimbizana mabao kwa mguu wa kushoto

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki na winga wa Azam FC, Gibrill Sillah, wanaongoza kwa kufunga mabao kwa kutumia mguu wa kushoto kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Takwimu za Bodi ya Ligi zinaonyesha kila mmoja amefunga mabao sita kwa mguu huo, sawa na mshambuliaji mwenzao wa Azam, Nassor Saadun, ambaye mabao yake yote sita ameyafunga kwa mguu wa kushoto pekee.

Sillah amefunga mabao manane hadi sasa, sita kwa mguu wa kushoto na mawili kwa mguu wa kulia, huku Aziz Ki akiwa na mabao saba, sita kwa mguu wa kushoto na moja kwa kichwa.

Wengine wanaofuatia kwa mabao ya mguu wa kushoto ni Offen Chikola wa Tabora United na Selemani Bwenzi wa KenGold, wote wakiwa na mabao matano.

Joshua Ibrahim wa Namungo amefunga manne kwa mguu wa kushoto kati ya mabao yake matano ya jumla msimu huu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *