Benki ya Stanbic imefanikiwa kuendesha droo ya pili ya mwezi ya kampeni yake ya Tap Kibingwa, ambapo washindi watano wamejishindia kiasi cha TZS 500,000 kila mmoja.

Kampeni hii inalenga kuchochea matumizi ya Kadi za Visa Debit kwa ajili ya miamala ya kidijitali, ikiendelea kuhamasisha urahisi na usalama wa malipo yasiyo ya pesa taslimu kote nchini Tanzania.
Washindi wa droo ya Machi ni:
✍️Richard Muyambo
✍️Alice Frank Mutagonda
✍️Saddam Ally
✍️Nabbila Abbasali Hirji
✍️Siddharth Misra
Meneja wa Kutoa Kadi wa Benki ya Stanbic, Irene Mutahibirwa, amesisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendeleza malipo ya kidijitali nchini Tanzania.
“Tap Kibingwa ni sehemu ya mkakati wetu mpana wa kuimarisha ubunifu wa kifedha na ujumuishi wa kifedha. Miamala ya kidijitali huleta usalama na ufanisi, na tunafurahia kuendelea kuwazawadia wateja wetu kwa kufanya maamuzi bora ya kifedha,” alisema Mutahibirwa.
Tap Kibingwa ni kampeni maalum inayoendeshwa na Benki ya Stanbic inayohamasisha wateja kutumia Kadi za Visa Debit kwa malipo ya kila siku badala ya pesa taslimu.
Wateja wanaofanya miamala ya angalau TZS milioni 5 kwa mwezi wanapata nafasi ya kushiriki kwenye droo za kila mwezi. Kampeni hii inaendelea hadi mwisho wa Machi 2025, ambapo droo kubwa itamshuhudia mshindi mmoja akiibuka na gari jipya aina ya Suzuki Fronx 2024, zero mileage.
Droo ya mwisho ya mwezi Machi inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huo, ikiwa ni hatua ya mwisho ya kampeni hii ya kipekee. Ushindi huu unaonyesha dhamira ya Benki ya Stanbic ya kukuza huduma za benki kidijitali, kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma zilizo salama, rahisi, na zenye manufaa.
Katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali, Benki ya Stanbic inawahamasisha wateja wengi zaidi kutumia kadi zao kwa malipo na kujipatia fursa ya kushinda zawadi nono katika droo zijazo.