Shirikisho la Taekwondo Tanzania limepata viongozi wapya kupitia uchaguzi uliofanyika Novemba 15 jijini Arusha.
Waliochaguliwa ni Ramoudh Abdallah (Rais), Abdullah Mwaluhanga (Makamu wa Rais), Joseph Mwashuya (Katibu Mkuu), Francisca Assey (Mweka Hazina) na viongozi wengine wa mashindano na ufundi.
Ofisa Michezo wa BMT, Charles Maguzu amewataka viongozi hao kuhimiza wanachama wao kulipa ada za uanachama ili watambulike rasmi. Pia amewashauri kufanya kazi kwa umoja na kusoma Katiba ili kuelewa majukumu yao ipasavyo.




