BOOST kinara mageuzi ya elimu Shule ya Msingi Mzizima

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mzizima Maua Kibendu, ameishukuru Serikali kupitia Mradi wa BOOST imewezesha ujenzi wa shule hiyo kuimarisha mazingira ya ujifunzaji.

Pia ameongeza kuwa BOOST imewezesha mafunzo kwa Walimu 16, hali iliyochagiza ufundisha na Ujifunzaji chanya kwa wanafunzi.

Mwanafunzi Abiero Odwar na Subra  Kumbata wameeleza kuwa miundombinu bora na vifaa vya kutosha katika shule yao vinawawezesha kujifunza kwa weledi.

Shule ya Msingi Mzizima imegharimu Sh. milioni 306.9 zilizotolewa na Mradi wa Kuimarisha na Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *