Chama cha Mapinduzi Kata ya kilimani kimeanza kusaka kura za wagombea wake wa mitaa minne kwa kupita nyumba kwa nyumba kunadi sera zao kwa wananchi ili wachaguliwe kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.

Katika Mtaa wa Nyerere na kilimani baadhi ya viongozi CCM wakiongozwa na Mjumbe wa kamati ya siasa wa kata hiyo, Barnabas kisengi pamoja na wagombea wao wanapita nyumba kwa nyumba baada ya kufanya mkutano wa hadhara wa kunadi sera zao.
Mgombea wa Mtaa Kilimani Janet Chibago na Mgombea wa Mtaa wa Nyerere, Lussy Rutainurya wamesema wanaamini watapata ushindi kwa kuwa wapo tayari kuwatumikia wananchi na sio kutanguliza maslahi yao binafsi.

