Chipukizi United yatimia nusu ya lengo Unguja

Kocha wa Chipukizi United, Mzee Abdallah, amesema timu yake imetimiza nusu ya lengo lao baada ya kushinda mechi moja kati ya mbili walizocheza visiwani Unguja.

Chipukizi walishinda mchezo mmoja na kupoteza mwingine dhidi ya Malindi SC kwa bao 1-0. Kocha huyo amesema walikosa makini katika umaliziaji licha ya kutengeneza nafasi nyingi.

Timu hiyo inarejea Pemba kurekebisha makosa ili kuhakikisha wanashinda mchezo wao ujao na kubaki salama katika msimamo wa ligi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *