COSTECH yataka kasi iongezwe ujenzi wa jengo la sayansi Dodoma

Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Kamisheni ya COSTECH, Prof. John Kondolo, amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) jijini Dodoma, ili likamilike Machi 2026 kama ilivyopangwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi, Prof. Kondolo alisema ameridhishwa na ubora na viwango vya ujenzi, akieleza kuwa jengo hilo litakuwa na hadhi ya kitaifa na kimataifa katika kuendeleza sayansi na teknolojia.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu, alisema serikali imetoa takribani Sh bilioni 8 kwa ujenzi huo, ambalo litakuwa na maabara, kumbi za mikutano na eneo la incubation kwa wabunifu.

Nungu alieleza kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutarahisisha uratibu wa shughuli za utafiti na teknolojia nchini kwa kuwa na miundombinu ya kisasa na mazingira bora kwa wataalamu.

Musanifu wa mradi, Benedict Martin, alisema jengo limebuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya kisayansi, ikiwa ni pamoja na ofisi, kumbi, maonyesho na mifumo ya mawasiliano ya kidigitali kwa matumizi ya muda mrefu.

Ujenzi wa jengo la STU unatarajiwa kuimarisha nafasi ya Tanzania katika utafiti na kukuza ushirikiano kati ya wanasayansi, wabunifu na sekta binafsi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *