Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Ngara, mkoani Kagera, umetaja ujenzi wa daraja la mawe la Mkajagari umefikia asilimia 95 ya utekelezaji.
Mara tu daraja hilo litakapokamilika, litaondoa adha ya mafuriko ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiwakabili wananchi wa Kata ya Mubumba na Bukiriro, hasa nyakati za mvua kubwa.

Wananchi wa maeneo hayo wamesema mradi huo ni suluhisho muhimu litakalowawezesha kusafiri kwa urahisi, kuimarisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.




