Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeHabariDk. Samia: Tanzania namba mbili uzalishaji mahindi Afrika

Dk. Samia: Tanzania namba mbili uzalishaji mahindi Afrika

Hatua ya Serikali kutoa ruzuku ya pembejeo na mbolea, Rais Dk Samia Suluhu Hassan amesema imeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa mahindi Afrika.

Kwa mujibu wa Dk Samia ambaye pia ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika mwaka huo, Tanzania imezalisha tani milioni 10 za zao hilo na kuzipiku nchi nyingi Afrika.

Dk. Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumapili Septemba 7, 2025 alipozungumza na wananchi wa Iringa Mjini, katika mwendelezo wa kampeni zake za urais zinazoendelea nchi nzima.

“Mkitupa ridhaa tutaendela kutoa ruzuku ya mbolea kote nchini pamoja na pembejeo, pia tutajenga vituo 50 vya kuhifadhia mazao ya parachichi na vingine 50 kwa ajili ya uhifadhi wa mazao ya mbogamboga,” amesema Dk. Samia.

Ameahidi kujenga maghala ya kuhifadhi mazao ya chakula na biashara na kuanzisha vituo vya ukodishaji wa zana za kilimo, ili wakulima wakodishe zana hizo kwa bei nafuu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments