“Ndugu zangu pamoja na hali hiyo ya kujiamini kwamba CCM ndio chama kikubwa na tuna matumaini makubwa kwenye uchaguzi ujao tusibweteke. Tunatimiza miaka 48 katika mwaka wenye vuguvugu za Uchaguzi Mkuu nchini. Kama nilivyosema kwenye Mkutano Maalum uliomalizika hivi karibuni, tusiruhusu kunyemelewa na kibri ya kuwabeza wapinzani wetu, lakini pia tusiingiwe na pepo la kuwaogopa,”Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Samia Suluhu Hassan.