“Ndugu zangu, kuaminika kwa Chama Cha Mapinduzi hakujatokea tu, bali ni matokeo ya jitihada za kushughulikia matatizo ya wananchi kupitia utekelezaji wa ahadi zake zilizomo kwenye ilani ya Uchaguzi. Ahadi za kujenga uchumi imara, kuimarisha huduma za kijamii, kujenga miundombinu mbalimbali na kujenga mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji vyote hivyo vimekuwa ni kete ya imani ya chama ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi,” Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan.