Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko anawaalika Wadau wa Matumizi Bora ya Nishati katika Mkutano wa Kikanda (REEC2024) utakaofanyika Jijini Arusha tarehe 4 na 5 Desemba, 2024.
Mkutano huo utahusisha Wadau mbalimbali kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).