Sunday, October 12, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Tunajenga uzio kudhibiti mamba Ziwa Victoria

Dkt Samia: Tunajenga uzio kudhibiti mamba Ziwa Victoria

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake inajenga uzio ndani ya Ziwa Victoria, kudhibiti mamba wasiwadhuru wananchi wanapotumia ziwa hilo kwa huduma nyingine.

Sambamba na hatua hiyo, amesema kwa miaka mitano iliyopita amefanikisha ujenzi wa vizimba 400 ziwani humo na kuwanufaisha vijana na ufugaji Samaki.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Agosti 7, 2025 alipozungumza na wananchi wa Misungwi mkoani Mwanza, katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Kwa kuwa anatambua katika Ziwa Victoria kuna mamba, Serikali yake imeanza kujenga uzio kuwaweka pembeni wanyama hao na kutenga maeneo ambayo wanawake na wananchi wengine watayatumia kufanya shughuli zao.

Kuhusu vizimba vya samaki, amesema katika miaka mitano ijayo ataongeza ujenzi wa vizimba na kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi, pia ataanzisha viwanda vya kuchakata samaki.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments