Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeMichezoDR Congo yaibwaga Nigeria kwa Penalti

DR Congo yaibwaga Nigeria kwa Penalti

šŸ“ŒYaongeza Matumaini ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026

DR Congo imeongeza matumaini yake ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuiondoa Nigeria kwa ushindi wa 4-3 kupitia mikwaju ya penalti, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 katika fainali ya mchujo wa Afrika.

Nahodha wa Leopards, Chancel Mbemba, alihakikisha timu yake inavuka hatua hiyo kwa kufunga penalti ya mwisho, baada ya kipa Timothy Fayulu kuokoa mkwaju wa beki Semi Ajayi katika mzunguko wa sita na kuwaweka Super Eagles katika presha kubwa.

Ushindi huo unaifikisha DR Congo kwenye hatua ya mwisho ya mchujo wa baina ya mabara, itakayochezwa Machi mwaka ujao, hatua ambayo itakuwa ya mwisho kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kwa upande wa Nigeria, matokeo hayo ni pigo jingine kubwa, kwani Super Eagles watakosa kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo, baada ya mchezo uliowaacha wakionekana kukosa ubunifu na uimara katika dimba la Rabat.

Nigeria ilianza vizuri dakika ya tatu kupitia shuti la Frank Onyeka, lililoguswa na mchezaji mwingine na kumfanya kipa achanganyikiwe. Hata hivyo, DR Congo haikusita kujibu.

Mshambuliaji Meschack Elia aliisawazishia Leopards kwa kumalizia kwa ustadi kutoka karibu, dakika chache baada ya kutimia nusu saa ya mchezo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments