“Endeleeni kuelimisha umma kuhusu shughuli za Ofisi ya Waziri Mkuu”- Katibu Mkuu Agnes

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Agnes Meena ametoa rai kwa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utendaji wa taasisi na programu mbalimbali zinazosimamiwa na Ofisi hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 02, 2025 alipotembelea banda la Ofisi hiyo akiwa ameambatanan na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dk. Stephen Nindi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri katika Maonesho ya Naneane yanayofanyika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

“Wananchi wanauhitaji Mkubwa wa kufahamu shughuli zinazoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo kuna umuhimu wa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma,” ameeleza.

Maonesho ya Wakulima maarufu Nanenane yamebebwa na kauli mbiu isemayo: “Chagua Viongozi Bora, kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *