Tuesday, February 3, 2026
spot_img
HomeBiashara‎EWURA yatangaza bei za mafuta Februari 2026, dizeli yashuka maradufu

‎EWURA yatangaza bei za mafuta Februari 2026, dizeli yashuka maradufu

DODOMA: 4 Februari 2026: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa  za mafuta aina ya petroli zitakazotumika hapa nchini kwa mwezi kuanzia tarehe 4 Februari  2026, zikionesha kushuka maradufu  kwa bei ya dizeli kwa mafuta yaliyopokelewa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

‎Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Mwainyekule, leo 4 Februari 2026, imebainisha kuwa, bei ya rejareja ya petroli dizeli imepungua  kwa Sh. 90 kwa mafuta yaliyopokelewa Dar es Salaam, 25 kwa Tanga na shilingi 24  kwa bandari ya Mtwara. Aidha, bei ya mafuta ya taa nayo imepungua kwa  Sh. 17, 14 na 93 kwa mafuta yaliyopokelewa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia ikilinganishwa na bei za mwezi Januari 2026.

‎Hivyo basi, bei za reja reja za bidhaa za mafuta kwa mwezi huu, zitakuwa Sh. 2,788, 2,849 na 2881  kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia. Na bei ya dizeli, Dar es Salaam ni Sh. 2,701, Tanga 2,762  na Mtwara 2,807 huku bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam ikiwa ni Sh. 2,881, Tanga 2794 na Mtwara  2,838.

‎Aidha, kwa mwezi Februari 2026, gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam ziliongezeka kwa wastani  1.88% kwa mafuta ya petroli na 1.65% kwa mafuta ya taa na kupungua kwa wastani wa  5.10% kwa mafuta
‎ya dizeli. Kwa bandari ya Tanga zimepungua kwa  1.62% kwa petroli na dizeli; huku  bandari ya Mtwara zikipungu kwa 9.24% kwa mafuta ya petroli. Vilevile, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umeongezeka kwa  1.86%.

‎ EWURA inawahimiza wauzaji wa mafuta nchini kutoa stakabadhi za mauzo kwa wanunuzi zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Aidha,vituo vyote vya mafuta nchini vichapishe bei za bidhaa za mafuta  katika mabango yanayoonekana bayana kwani kutokufanya hivyo ni kosa  na atakayekiuka atapata adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments