EWURA yawaita wadau Kigoma kuwekeza vituo vya mafuta vijijini

Meneja EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher, amewataka wadau wa masuala ya uuzaji wa mafuta kutumia fursa ya kuwekeza katika maeneo ya vijijini ambako kuna uhaba mkubwa wa vituo vya mafuta.

Mhandisi Christopher ametoa wito huo kwenye mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani Kasulu – Kigoma.

Naye, Mwenyekiti wa wauzaji wa mafuta wa Wilaya ya Kigoma, Salum Ally ameipongeza EWURA kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wadau wa mafuta na kusema kwamba zoezi hilo liwe endelevu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *