Gunners FC ya Dodoma imefanikiwa kupanda Ligi ya Championship baada ya kuichapa Mapinduzi FC mabao 2-1 kwenye mchezo wa First League uliochezwa Uwanja wa CCM Samora, Iringa.

Matokeo hayo yameiwezesha Gunners kuongoza Kundi B kwa pointi 45, ikifuatwa na Tanesco FC (32) na Rhino Rangers (31). Gunners inajiunga na Hausung ya Njombe, ambayo ilitangulia kupanda daraja.
Wakati huo huo, Mtibwa Sugar inaongoza Ligi ya Championship kwa pointi 60 na inahitaji pointi 11 pekee kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Mbeya City na Stand United zikipambana kuwania nafasi ya pili.