Habari

Mkutano wa 45 wa Wakuu wa nchi wa SADC waanza Madagascar

Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeanza Agosti 04, 2025 jijini Antananarivo, Madagascar na Kikao cha Wataalamu cha Maafisa Waandamizi cha kupitia Utekelezaji wa Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa Kikanda 2030 (Regional Indicative Strategic Development Plan 2030-RISDP). zania inashiriki kikao hicho muhimu kwa maendeleo […]

Mkutano wa 45 wa Wakuu wa nchi wa SADC waanza Madagascar Read More »

REA yapongezwa kwa kutoa mikopo nafuu ya ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepongezwa kwa utekelezaji wa Mradi wa Mkopo Nafuu wa Ujenzi wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini ambapo utekelezaji wake umetajwa kuwa kichocheo cha maendeleo ya Watu wa vijijini. Akitoa pongezi hizo; Katibu Tawala wa wilaya ya Ikungi, Rashid Rashid ambaye ametembelea banda wa REA leo,

REA yapongezwa kwa kutoa mikopo nafuu ya ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta vijijini Read More »

Wastaafu PSSSF waelezwa umuhimu wa kuhakiki majina kwenye taarifa zao

Wastaafu wanaopokea Pensheni kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamekumbushwa kuwa endapo mstaafu anahitaji kufanya mabadiliko ya majina yake anapaswa kufanya hivyo ndani ya miezi mitatu ya kustaafu kwake. Hayo yameelezwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, Rajabu Kinande, wakati akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwenye Maonesho

Wastaafu PSSSF waelezwa umuhimu wa kuhakiki majina kwenye taarifa zao Read More »

Majaliwa awapongeza vijana wanaofuga samaki kwa vizimba

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewapongeza vijana wanaojiajiri kwa kufuga samaki kwa kutumia vizimba na kutaka wengine waige mfano huo. Ametoa pongezi kwa vijana hao leo alipotembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB na kukuta simumizi za vijana hao ambao wameweza kufuga samaki na kuingiza faida ya mamilioni. Majaliwa amesema vijana hao wanatakiwa kushikwa

Majaliwa awapongeza vijana wanaofuga samaki kwa vizimba Read More »

NEMC yapigia chapuo kilimo hifadhi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewakumbusha wawekezaji kuhakikisha wanakuwa na cheti cha tathmini ya mazingira (EIA) kabla ya kufanya uwekezaji wowote. Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kati-Dodoma, Novatus Mushi, wakati akitoa elimu kwa umma kwenye maonyesho ya wakulima yanayoendelea katika viwanja vya

NEMC yapigia chapuo kilimo hifadhi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Read More »

Wizara ya Nishati, Taasisi zake zashiriki Maonesho ya Kimataifa ya kilimo Dodoma

Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki Katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ambayo yameanza Tarehe 1 Agosti Katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma. Maonesho hayo yamebebwa na kaulimbiu iya ” Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025″, Katika maonesho hayo ambayo yamefunguliwa na Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdor

Wizara ya Nishati, Taasisi zake zashiriki Maonesho ya Kimataifa ya kilimo Dodoma Read More »

NMB yajidhatiti kusaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kupitia maonesho ya Nane nane

Mkuu wa Kitengo cha Biashara Serikalini kutoka Benki ya NMB, makao makuu, Vicky Bishubo, amesema wamepanga kutumia maonesho ya wakulima Nane nane kutoa elimu kwa wananchi kutambua fursa zinazotolewa na benki hiyo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini. Bishubo, alisema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya wakulima kitaifa katika viwanja vya

NMB yajidhatiti kusaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kupitia maonesho ya Nane nane Read More »

Katibu Tawala Singida aitaka TVLA kuwafikia wafugaji vijijini

Na Daudi Nyingo, Dodoma Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma R. Mganga, ameitaka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kuongeza juhudi za kuwafikia wafugaji wadogo waishio vijijini ili kutambua changamoto wanazokutana nazo hususan katika suala la uchanjaji wa mifugo. Dk. Mganga ametoa wito huo leo Agosti 2, 2025, alipotembelea banda la TVLA lililopo

Katibu Tawala Singida aitaka TVLA kuwafikia wafugaji vijijini Read More »