Makardinali wanatarajiwa kukutana siku ya leo ili kuamua tarehe ya mazishi ya Papa Francis, aliyefariki dunia siku ya Jumatatu Vatican, akiwa na umri wa miaka 88, baada ya kupatwa na kiharusi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Kitume, mazishi ya Papa yanapaswa kufanyika kati ya siku ya nne hadi ya sita baada ya kifo chake. Hata hivyo, maamuzi ya mwisho yatafanywa na makardinali.