Sunday, March 22, 2026
spot_img
HomeMichezoIOC yaitaka TOC kufanya uchaguzi

IOC yaitaka TOC kufanya uchaguzi

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imeiandikia barua Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ikiitaka ifanye uchaguzi mkuu ifikapo mwishoni mwa Septemba 2025.

Rais wa TOC, Gulam Rashid, amesema wamelipokea ombi hilo na wanatarajia kuomba uchaguzi huo usogezwe kwa wiki moja ili upishane na Mkutano Mkuu wa IOC kanda ya Afrika utakaofanyika Msumbiji.

Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau, amesema uchaguzi huo utafanyika kwa kufuata Katiba ya IOC, na baada ya taratibu kukamilika watatoa taarifa rasmi kwa Watanzania kuhusu tarehe ya uchaguzi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments