Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira inayoongozwa na Mwenyekiti Jackson kiswaga imeridhishwa na ujenzi wa bwawa la maji katika kijiji cha Kizengi wilaya ya Uyui mkoani Tabora .

Kwaniaba ya kamati hiyo Mwenyekiti wa kamati Mhe kiswaga amesema wameridhishwa na Ujenzi wa Mradi huo na kuipongeza Wizara ya Maji kwa kazi nzuri ya ujenzi wa Bwawa hilo na mabwawa mengine nchini ambapo pia amesisitiza ujenzi wake uende kwa kasi ili wananchi waweze kupata huduma ya majisafi na salama.
Mhe Kiswaga amezungumza hayo alipotembelea eneo linapo jengwa bwawa hilo ili kujionea utekelezaji wake unavyo endelea
Bwawa hili linalojengwa kwa fedha za ndani linagharimu zaidi ya bilioni 4 linauwezo wa kuhifadhi maji kwa mwaka lita bilioni 5.1 na litanufaisha wananchi zaidi ya 90,000 na kwasasa limefia asilimia 60 ya utekelezaji wake.




Aidha Kamati imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta seti tano za mitambo ya uchimbaji wa mabwawa ili kuweza kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali nchi
Aidha kamati hiyo imempongeza Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso na wataalam kwa kazi ya kuwafikishia wananchi huduma ya majisafi .


