Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha leo, Machi 28, 2025, imekabidhi kompyuta kwa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha ili kusaidia matumizi ya mifumo ya kisasa inayotumiwa na kikosi hicho katika utoaji wa huduma.

Kompyuta hizo zimekabidhiwa na Mjumbe wa Kamati hiyo, Bi. Veronica Ignatus, na kupokelewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo, SSP Zauda Mohamed. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa wa polisi, wakaguzi na askari wa kikosi hicho.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika maboresho ya utendaji ndani ya kikosi hicho, ambacho kwa sasa kimejikita zaidi katika matumizi ya mifumo ya kidigitali kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.



