Tuesday, March 17, 2026
spot_img
HomeHabariKampeni yarejesha matumizi ya mti ya mswaki

Kampeni yarejesha matumizi ya mti ya mswaki

Wakati takwimu za kitaifa zikionesha asilimia 76.5 ya Watanzania wanakabiliwa na changamoto ya kung’oa meno kutokana na kuoza, wadau wa mazingira nchini wameanza kupiga debe kurejeshwa kwa matumizi asili ya ‘miti ya miswaki’ yenye kimiminika cha madini ya floride inayopatikana kwenye mimea ili kudhibiti hali hiyo.

Akizungumza jana Machi 16, 2026 katika Shule ya Sekondari Bomambuzi iliyoko Kata ya Kaloleni, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, Dismas Mlaki, ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Kili Climate Day, amesema wamekuja na kampeni hiyo kwa sababu matumizi ya miswaki ya plastiki kwa miaka mingi imeonesha haina rutuba kwenye meno.

“Tunahimiza matumizi ya miti ya miswaki, kwa sababu mti mswaki, ni mti ambao una rutuba ambayo ina liquid ya floride unapotumia kubrashia meno yako. Tunatumia hicho kijiti kwa mwezi mmoja, miwili na hatuathiri mti. Kwa kuanzia kampeni yetu, tumeamua kuwafikia wanafunzi zaidi ya 1,500 katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Zaidi ameongeza, “Program ya tooth brash hygene, ni mahususi kwa ajili ya kuelezea namna bora ya kuweza kutumia ‘mti mswaki’ kama chanzo bora cha uimara kwa meno. Kwa hiyo kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia miswaki ya plastiki na mababu na mabibi zetu, walitumia miti hii ya miswaki ya miti kusaidia meno kwa kuzuia bakteria na meno kuwa imara zaidi.”

Mradi huo uko chini ya usimamizi wa Taasisi ya Jane Goodall Roots & Shoots na unatekelezwa na Shirika la Green Manjaro Foundation ikishirikiana na Taasisi ya PHARUS ya Nertheland.

Kwa mujibu Mlaki, mti mswaki haina athari za kimazingira, kwa sababu mti haukatwi ila unapunguzwa matawi madogo madogo na shina linaendelea kubaki na kuuendelea kuchipua tena matawi mengine. 

Aidha, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bomambuzi, Titus Ngulai, akielezq namna alivyoguswa na kampeni hiyo, amesema miti ya miswaki inafanya meno kuweza kuimarika na kuwa imara zaidi tofauti na mtu anayetumia mti wa plastiki.

‘Ni kweli miti mswaki, ndiyo iliyofanya wazee wetu wakawa na meno imara kwa miongo mingi, tofauti na sasa vijana wanang’oa meno katika umri mdogo.Ushauri wangu kwa jamii ni tulinde asili ambayo tuliachiwa.Turejeshe miti miswaki na misitu iliyoharibiwa na usasa. Mti mswaki ni mti bora na ni mzuri kwa afya ya kinywa.”ameisema.

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bomambuzi, Joy Julius, amesema vijana hasa wanafunzi, ndio kundi ambalo liko tayari kuchangia mabadiliio hapa nchini, ikiwamo kulinda ikolojia ya Mlima Kilimanjaro.

“Mti kwa kawaida unakuwa na maji yake asilia, ambayo husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya. Kuna mimea ambayo ukiweza kuitumia kinywa huwa hakitoi harufu mbaya, hasa wanaopitia changamoto ya jino kupekechwa. Tumejifunza namna ya miti inavyotusaidia kusafisha meno yetu,”ameeleza mwanafunzi huyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno wa Wizara ya Afya,  Watanzania wanaotishiwa na changamoto ya kuoza meno, wamefikia asilimia 76.5

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments