Friday, March 20, 2026
spot_img
HomeHabariKatambi ataka uboreshaji mifumo utoaji huduma kwa wafanyabiashara

Katambi ataka uboreshaji mifumo utoaji huduma kwa wafanyabiashara

Naibu Waziri wa Viwanda,Patrobas Katambi ameiagiza menejimenti ya wizara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhakikisha wanaimarisha sera ,sheria pamoja na kuboresha mifumo ya usimamizi wa biashara ili kupunguza urasimu usio wa lazima katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema sekta binafsi si mshindani wa biashara bali ni sekta muhimu katika safari ya utatuzi wa changamoto katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.

Amebainisha hayo kwaniaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha menejimenti kilicholenga kujadili na kufanya tathmini ya utendaji wa Wizara na taasisi zake, Januari 8, 2026 Jijini Arusha.

Naibu Waziri Katambi amesema uboreshaji wa mifumo na taratibu za udhibiti na usimamizi wa biashara , mifumo lazima iwe rahisi ikiwemo kuendeleza majadiliano ya mara kwa mara na wadau wa sekta binafsi ili sera ziwe shirikishi na zenye kutatua changamoto za wafanyabiashara.

Aidha amesema huduma zinazotolewa kwa wafanyabiashara na wawekezaji zinapaswa kuwa na uwazi ikiwemo ushirikishwaji sekta binafsi katika kupendekeza maboresho ya mifumo na mabadiliko ya sheria ili kuondoa vikwazo vinavyolalamikiwa na wadau wa biashara

Naibu Waziri Katambi amesema Ushirikiano wa karibu baina ya wizara, taasisi na sekta binafsi ni muhimu kwani sekta binafsi sio mpinzani wa serikali bali ni mshiriki muhimu katika safari ya maendeleo ya uchumi wa taifa

Naye Katibu Mkuu wa Wizara Dk. Hashil Abdallah amesisitiza kikao hicho ni muhimu katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa na menejimenti yanafika ikiwemo kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda, kukuza ajira, upatikanaji wa mitaji ikiwemo ubunifu na uvumbuzi katika kuhakikisha sekta ya viwanda inaimarika zaidi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments