Kocha Mayanga aanza na kipigo Mashujaa FC

Na Mwandishi Wetu

Kocha mpya wa Mashujaa FC, Salum Mayanga, ameanza rasmi majukumu yake kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa Pamba Jiji kwenye mchezo wa 16 bora wa Kombe la FA, uliopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Mayanga, aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Mohamed Abdallah ‘Bares’ baada ya matokeo mabaya ya timu, ametokea Mbeya City, aliyokuwa akiiongoza kabla ya kujiunga na Mashujaa.

Bao pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 45 na Alain Mukeya, akiunganisha krosi ya Deus Kaseke. Mayanga alieleza kuwa licha ya kutengeneza nafasi tano, walishindwa kuzitumia huku wapinzani wakizuia vyema kipindi cha pili.

Kocha wa Pamba Jiji, Fred Minziro, alisema walishinda kwa nidhamu na kuheshimu ubora wa Mashujaa FC.

Pamba Jiji sasa inaungana na Simba, Yanga, Stand United, JKT Tanzania, Singida United, Kagera Sugar na Mbeya City kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la FA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *