Kocha wa Yanga aapa kulipa kisasi dhidi ya Tabora United

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, ameweka wazi kuwa timu yake lazima ishinde dhidi ya Tabora United kwenye uwanja wao wa nyumbani kesho, ili kulipa kisasi cha kufungwa 3-1 katika mchezo wa kwanza Novemba 7, mwaka jana.

Hamdi amesema wachezaji wa Yanga wanatambua umuhimu wa mechi hiyo na wanawajibika kurejesha furaha kwa mashabiki baada ya machungu ya kufungwa awali.

Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Yanga kushinda 2-0 dhidi ya Songea United katika hatua ya 16 bora ya Kombe la FA, na kufuzu robo fainali. Hamdi amepongeza wachezaji wake kwa kutoonyesha makosa binafsi na pia kumsifu kipa wa Songea United, Khatib Mbwana, kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.

Kocha wa Songea United, Meja Mstaafu Abdul Mingange, amesema waliheshimu Yanga lakini hawakuwapa wachezaji wake presha ya kushinda, bali walitaka wacheze mpira mzuri. Pia, alimpongeza kipa wake Mbwana, aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana cha Coastal Union.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *