Monday, March 16, 2026
spot_img
HomeHabariKombo aapishwa Mbunge Bunge Afrika

Kombo aapishwa Mbunge Bunge Afrika

Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) leo Machi 16, 2026 katika mkutano maalum wa Bunge la Tano la jumuiya hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao (virtual).

Waziri Kombo ameapishwa kuwa mbunge kwa wadhifa wake wa uwaziri (ex-officio), hatua inayomruhusu kushiriki katika shughuli za bunge hilo kwa mujibu wa taratibu za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5(4) ya Kanuni za Bunge la Afrika Mashariki, mbunge haruhusiwi kuketi au kushiriki katika shughuli za bunge hilo bila kwanza kula kiapo cha utii kwa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuapishwa kwa Kombo kunamwezesha kuanza rasmi majukumu yake katika bunge hilo la kikanda, ambalo linahusisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kushughulikia masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments