Joan Laporta amechaguliwa tena kuwa Rais wa Barcelona kwa muda wa miaka mitano baada ya kumshinda, Victor Font, katika uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia jana.
Laporta alishinda kwa kishindo, akipata kura 32,934 kati ya kura 48,480 kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo huku mpinzani wake, Font akiambulia kura 14,385.
“Kwanza kabisa, nataka kutoa maneno machache ya shukrani kwa klabu hii nzuri tuliyo nayo,” alisema Laporta baada ya ushindi wake kuthibitishwa.
“Ni vizuri kuona wanachama bado wanaweza kumchagua nani anayetuwakilisha. Shauku hii ni furaha, inaifanya klabu kuwa maalum, kwa hiyo shukrani kwa Barça na wanachama wote waliopiga kura katika onyesho la demokrasia.”
Jumla ya kura zilizopigwa ziliwakilisha idadi ya waliojitokeza kushiriki katika uchaguzi huo ya asilimia 42.34%, Barça ilisema.
“Tutaendelea kuilinda Barcelona dhidi ya kila kitu na kila mtu. Miaka ijayo itakuwa ya kusisimua. Itakuwa bora zaidi maishani mwetu.”
CHANZO: ESPN




