Ligi Kuu Zanzibar inatarajiwa kurejea rasmi Aprili 10, 2025, baada ya kusogezwa mbele kutoka tarehe 5 kutokana na ukamilishaji wa miundombinu ya viwanja na kipindi cha mfungo wa Ramadhani.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim, amesema viwanja vya Cairo (Unguja) na Finya (Pemba) havikuwa na miundombinu bora kwa matangazo ya wadhamini, hali iliyosababisha kusitishwa kwa muda. Hata hivyo, ameahidi kuwa ligi itamalizika kwa wakati na kwa kuzingatia kanuni.