“Tunasikitishwa na matukio mbalimbali yaliyotokea. Na mimi niungane na viongozi wa dini kukemea matukio haya yaliyotokea. Niliseme tu, matukio haya yasihusishwe na vyama vya upinzani tu.
Yani tusiongelee kwamba tunakemea jambo hili kwa sababu vyama vya upinzani vina watu ambao wamepatwa na matukio haya halafu tukasahau na Chama Cha Mapinduzi kama nacho kimefanyiwa matukio haya.
Naomba niliweke wazi hili, tunapokemea tukemee wote kwa pamoja. Tunapoeleza kasoro hizi ni kwa wote. Kwa hiyo haiwezi kutokea mtu akakaa, akaandika statement yake kwamba kumetokea mauaji . Mauaji ukaeleza ya wafuasi wenu.
Tunalikemea kwa nchi nzima kwa maana mauaji, kujeruhusiwa kwa watu, kupigwa kwa watu ni kwa vyama vyote, “Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla.