Malale Hamsini kutua Mbeya City

Mbeya City, iliyoshinda 2-0 dhidi ya Stand United, inakaribia kumtangaza Malale Hamsini kuwa Kocha Mkuu kuchukua nafasi ya Salum Mayanga aliyekwenda Mashujaa FC.

Timu hiyo, inayoshikilia nafasi ya pili kwa alama 55, inaendelea kuwania kupanda Ligi Kuu msimu ujao. Msimamo wa ligi unaongozwa na Mtibwa Sugar yenye alama 60, huku Geita Gold na Stand United zikiwania nafasi ya tatu.

Timu mbili za juu zitapanda moja kwa moja, huku nafasi ya tatu na nne zikicheza mchujo kupata timu itakayomenyana na klabu ya Ligi Kuu kwa nafasi ya mwisho ya kupanda daraja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *