Martha Kivunge na Chiku Issa waibuka kidedea kura za maoni UWT Arusha

Wanasiasa mahiri Martha Kivunge na Chiku Issa wameibuka washindi katika kura za maoni za kusaka mgombea wa Ubunge wa Viti Maalum (UWT) Mkoa wa Arusha, baada ya kupata idadi kubwa ya kura katika uchaguzi uliohusisha wagombea wanane.

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Kihongosi, alitangaza rasmi matokeo yaliyowaweka Martha na Chiku juu ya wagombea wengine.

➡️ Martha Kivunge alipata kura 1,004
➡️ Chiku Issa alipata kura 775

Idadi ya wajumbe waliopiga kura ilikuwa 1,261, ambapo kura halali zilikuwa 1,245 na kura saba (7) ziliharibika.

Wagombea wengine walioshiriki na kura walizopata ni kama ifuatavyo:
• Catherine Magige – 213
• Asanterabi Lowassa – 196
• Zaytuni Swai – 141
• Navoi Mollel – 95
• Martha Amo – 50
• Lilian Badi – 9

Kwa mujibu wa matokeo hayo, waliokuwa wawakilishi wa UWT Mkoa wa Arusha waliomaliza muda wao na sasa hawakufanikiwa kurejea ni Catherine Magige na Zaytuni Swai.

Zoezi hilo limeelezwa kuwa la wazi, huru na la amani, huku wajumbe wakionyesha mshikamano na hamasa kubwa katika kuchagua viongozi wa kizazi kipya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *