Mbeya City imemsajili beki wa kati na nahodha wa Tabora United, Kingu Kelvin Pemba, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi kilichopanda Ligi Kuu Tanzania Bara.

Klabu hiyo pia ilimsajili beki Ibrahim Ame kutoka Mashujaa FC na kuongeza mikataba kwa washambuliaji Eliud Ambokile na Baraka Maranyingi.
Wachezaji 9 wakiwemo Kilaza Mazoea, Pius Joseph, Jeremiah Thomas, Fred Mlelwa na wengine wameachwa.
Habari za ndani zinadai klabu ipo mbioni kuwasajili wazoefu kama kipa Beno Kakolanya, straika Habib Kyombo (Singida Black Stars) na kiungo Sospeter Bajana (Azam FC).