Mfungaji bora Senegal atua Azam FC

Azam FC imemsajili kwa miaka miwili winga wa Senegal, Pape Doudou Diall, kutoka Generation Foot.

Diallo alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Senegal akiwa kwa mkopo Linguere de Saint-Louis, akifunga mabao 11.


Huyu ni mchezaji wa kwanza wa kigeni kutambulishwa na Azam msimu huu, na wa tano kwa jumla.

Wengine ni Himid Mao, Aishi Manula, Lameck Lawi na Muhsin Malima.
Azam FC ipo kambini chini ya kocha Florent Ibenge, ikijiandaa kwa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *