Kocha Mkuu wa Namungo, Juma Mgunda, amewahakikishia mashabiki wa soka mkoani Lindi kuwa timu hiyo haitoshuka daraja na watafanya kila jitihada kusalia Ligi Kuu.

Mgunda, aliyerithi kikosi kutoka kwa Mwinyi Zahera, ameiongoza Namungo kushinda michezo minne, sare moja na kupoteza saba kati ya 16 alizoongoza. Timu hiyo ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 23, ikihitaji matokeo mazuri katika mechi saba zilizosalia ili kuepuka kushuka daraja au mechi za mchujo.
Kesho, Namungo itavaana na Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza katika mzunguko wa 23 wa Ligi Kuu.