Michezo

JKU Princess kujipanga kwa CECAFA

JKU Princess ya Zanzibar itaanza kambi Jumatatu kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayofanyika Septemba 4–12 jijini Nairobi. Timu itapiga kambi Dar es Salaam au Dodoma kwa ushirikiano na Fountain Gate, ili kupata mechi za kirafiki zenye ushindani. Katibu Shazil Khatibu amesema wataongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi na kuweka historia

JKU Princess kujipanga kwa CECAFA Read More »

Josiah Karibia kujiunga na Namungo

Namungo FC ipo kwenye hatua za mwisho kumtangaza Kocha wa Prisons, Amani Josiah, kuchukua nafasi ya Juma Mgunda aliyeondoka baada ya kumalizika kwa mkataba. Josiah aliiokoa Prisons kwenye ‘play off’ dhidi ya Fountain Gate na anasifika kwa kufundisha soka la kisasa. Namungo imeachana na wachezaji 11 na inatarajia kumtambulisha Josiah mara baada ya makubaliano na

Josiah Karibia kujiunga na Namungo Read More »

Morocco: “Kazi ndio inaanza”

📌Baada ya Taifa Stars kutinga Robo Fainali CHAN 2024 Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman “Morocco”, amesema safari yao kwenye CHAN 2024 ndio inaanza licha ya kufuzu robo fainali wakiwa na pointi tisa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Jamhuri ya Kati. Amesema hatua za juu ndizo zenye ugumu zaidi hivyo watalazimika kupambana mara mbili.

Morocco: “Kazi ndio inaanza” Read More »

Mlandege yaachana na wachezaji 5

Mlandege SC, wawakilishi wa Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wametangaza kuachana na wachezaji watano akiwemo Ally Mohamed Njiwa na Benson Young. Mmiliki wa timu, Abdulsatar Daud, amesema wameamua kuachana nao kutokana na kushuka kwa viwango na mpango wa kuunda kikosi chenye ushindani kwa msimu wa 2025/26, wakianzia kwenye michuano ya kimataifa.

Mlandege yaachana na wachezaji 5 Read More »