Mikakati ya Rais Samia, Tanzania kuwa namba moja uzalishaji wa chakula Afrika 

Rais Samia Suluhu Hassan ameelezea dira yake ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika kupitia mikakati mitatu mikuu ya serikali katika sekta ya kilimo.

Akiwa nchini Marekani jana aliposhiriki kwenye mjadala kuhusu kilimo barani Afrika katika mji wa Des Moines, Iowa, Rais Samia amesisitiza kuwa serikali yake imejizatiti kukuza sekta ya kilimo ili kufikia lengo hilo.

Katika maelezo yake, Rais Samia amebainisha mikakati mitatu muhimu ya kuendeleza kilimo ikiwemo uwekezaji katika Miundombinu ya Umwagiliaji

Amesema serikali imepanga kuwekeza katika miradi mikubwa ya umwagiliaji ili kuhakikisha ardhi nyingi zaidi inakuwa na uwezo wa kuzalisha mazao kwa mwaka mzima. Hii inalenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi wa mvua.

Mkakati wa pili alisema ni kuboresha upatikanaji wa teknolojia na pembejeo za Kisasa lengo ni kuongeza tija na ubora wa mazao.

Rais Samia amesema serikali inashirikiana na wadau wa maendeleo kutoa teknolojia za kisasa na pembejeo kwa wakulima.

“Hii itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mazao bora yenye thamani kubwa kwenye masoko ya ndani na nje,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema mkakati wa tatu ni kukuza masoko ya mazao ya kilimo tayari serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha mazao yanayozalishwa nchini yanapata masoko ya ndani na nje, na hivyo kuwapa wakulima faida zaidi kutokana na juhudi zao.

Rais Dkt. Samia alieleza kuwa mikakati hiyo Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika na hivyo kuchangia zaidi kwenye usalama wa chakula katika kanda nzima.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *