MOI yatoa zawadi za x-mas kwa watumishi 1,052, kuwatia hamasa

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imekabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watumishi wake 1,052, ikiwa ni sehemu ya kuwapa motisha na kutambua mchango wao katika utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Zawadi hizo, zenye thamani ya Tsh. 50,000 kwa kila mtumishi, zilikabidhiwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Mpoki Ulisubisya, kwa wawakilishi wa watumishi hao. Zilijumuisha kilo 15 za mchele, lita 2 za mafuta ya kupikia, na vinywaji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Dkt. Mpoki alisema zawadi hizo ni ishara ya shukrani kwa juhudi kubwa za watumishi wa MOI katika kuwahudumia wagonjwa.

“Menejimenti ya MOI tumetoa zawadi hizi kwa kutambua mchango mkubwa wa watumishi wetu katika huduma za matibabu. Tunawaomba msheherekee Sikukuu kwa amani na furaha,” alisema Dkt. Mpoki.

Mhudumu wa Afya wa MOI, Amina Makunga, aliishukuru menejimenti kwa zawadi hizo, akisema kuwa zinawapa ari na motisha zaidi ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *