Mrema, aeleza masikitiko yake kuhusu taarifa ya CHADEMA shambulio kiongozi BAWACHA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, ameonyesha masikitiko yake makubwa kuhusu taarifa iliyotolewa na chama chake juu ya tukio la kupigwa na kuumizwa kwa kiongozi wa wanawake wa chama hicho, tukio ambalo lilihusisha mwanaume.

Katika maelezo yake, Mrema amesema kuwa taarifa hiyo ya chama imetolewa kwa kuchelewa na imekosa mambo ya msingi, ambayo ni pamoja na:

  1. ✍️Kutokulaani tukio la ukatili – Chama hakikuona haja ya kulaani kitendo cha kiongozi huyo wa wanawake kupigwa, bali kimeeleza kuwa hizo ni taarifa zinazosambazwa mitandaoni.

2.✍️ Kutokutoa pole kwa mgonjwa – Chama hakijaonesha mshikamano kwa kiongozi wake aliyeathirika. Hali hii imezua maswali kwa kuwa chama hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa pole kwa viongozi wa vyama vingine wanapopatwa na majanga.

  1. ✍️Vitisho kwa mgonjwa – Badala ya kuonesha mshikamano, chama kimeonekana kumtisha mgonjwa na hata kupanga ni nani anapaswa kumpa faraja na nani haruhusiwi. Wakati huo huo, chama hakijaonyesha utayari wa kusaidia matibabu yake.
  2. ✍️Kauli zenye utata kuhusu uchunguzi – Chama kimedai kuwa kinaendelea na uchunguzi, lakini kinatoa vitisho kwa mgonjwa. Mrema amehoji iwapo mtu anayetishwa anaweza kutoa ushirikiano kwenye uchunguzi huo, hasa ikizingatiwa kuwa chama kimesema kuwa ni “tuhuma za mtandaoni.”

5.✍️ Msimamo unaofanana na enzi za utawala wa zamani – Mrema amefananisha matamshi ya chama na kauli zilizotolewa wakati wa utawala uliopita, ambapo watu walipopotea au kufanyiwa ukatili, majibu yaliyotolewa yalikuwa ni kuwataka watu waendelee na shughuli za maendeleo badala ya kuhoji matukio hayo.

Kwa mujibu wa Mrema, kitendo cha kumpiga kiongozi wa wanawake ni ukatili wa kijinsia ambao haupaswi kuvumiliwa. Ameitaka jamii kupinga na kukemea aina yoyote ya ukatili dhidi ya wanawake, ndani na nje ya vyama vya siasa.

“Ukatili huu hauna tofauti na manyanyaso yanayofanywa kwa wanawake wengine nchini. Ni jukumu letu wote kupinga matendo haya bila kujali nani ametendewa,” amesema.

Katika kuhitimisha kauli yake, amewatakia waumini wote wa dini ya Kiislamu heri ya Sikukuu ya Eid.

Eid Mubarak!

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *