Mtanda: Nimetimiza ahadi, Pamba Jiji haishuki daraja

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amesema ametimiza ahadi yake ya kuhakikisha Pamba Jiji haishuki daraja baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Bao pekee lilifungwa na Zabona Mayombya.

Mtanda amesema sasa lengo ni kuhakikisha timu inakwepa mchujo kwa kushinda mechi ijayo dhidi ya KMC: “Tumekubaliana na vijana kuhakikisha tunamaliza ligi salama bila kushiriki mechi za mchujo.”

Hadi sasa, Pamba Jiji ina pointi 33, sawa na Tanzania Prisons ikiwa itashinda mechi yake ya mwisho. Fountain Gate ipo nafasi ya 14 na inaweza kufikisha pointi 32 ikishinda. Pamba inahitaji sare dhidi ya KMC ili kufikisha pointi 34 na kujihakikishia kubaki Ligi Kuu.

KenGold na Kagera Sugar tayari zimeshuka daraja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *