Namungo yapata mbadala wa Nyoni

Klabu ya Namungo ipo kwenye mazungumzo ya kumchukua beki Jackson Shiga kutoka Fountain Gate ili kuziba nafasi ya Erasto Nyoni aliyeachwa na timu hiyo. Shiga alijiunga na Fountain Gate msimu uliopita akitokea Coastal Union.

Aidha, Namungo tayari imewasajili Abdallah Mfuko kutoka Kagera Sugar na Hussein Kazi wa Simba kuchukua nafasi ya Derrick Mukombozi (Burundi) aliyeachwa pia.

Mratibu wa klabu hiyo, Ally Suleiman, alisema tayari wamekamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji wapya, na hivi karibuni wataanza utambulisho rasmi. Wengine waliosajiliwa ni Abdallah Denis ‘Viva’, kiungo Lucas Kikoti aliyeonekana kurejea kikosini kutoka Coastal Union, pamoja na washambuliaji watatu: Heritier Makambo, Cyprian Kipenye na Abdulaziz Shahame.

Namungo imeachana na jumla ya wachezaji tisa, akiwemo straika Meddie Kagere na wengine kama Issa Abushehe, Joshua Ibrahim, Erick Kapaito, Erick Malongi, Emmanuel Charles na Anderson Solomoni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *