NBC yawashukuru wadau wa Dodoma Marathon


Benki ya NBC imewashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha mbio za sita za Dodoma Marathon zilizohusisha washiriki zaidi ya 12,000 na kuchangisha Sh milioni 700 kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto.

Akitoa shukrani, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, alimpongeza Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko na viongozi wengine kwa kushiriki tukio hilo, sambamba na wadhamini wakuu kama GSM Group, Sanlam, Vodacom, Jubilee Allianz, TBL na Wasafi Media.

Sabi alisema katika miaka mitano ya marathon hizo, zaidi ya Sh bilioni 1 zimesaidia miradi ya afya ikiwemo wanawake 47,000 kupimwa saratani ya shingo ya kizazi, wanafunzi 100 wa ukunga kufadhiliwa, pamoja na vifaa tiba kutolewa hospitalini kupitia ushirikiano na Ocean Road, Mkapa Foundation na AMREF.

Kwa mwaka huu, NBC inalenga kupima wanawake 10,000, kufadhili wakunga 100 zaidi na kuanzisha mpango wa masomo kwa wauguzi 100 wa watoto wenye usonji, kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *